CHINA : KAMPUNI ya Novo Nordisk imezindua dawa ya kupunguza uzito ya Wegovy nchini China baada ya kuidhinishwa na mamlaka ya afya mwezi Juni.
Zaidi ya watu milioni 180 wanaishi na uzito wa kupindukia nchini China ambapo kuna idadi ya watu wasiopungua bilioni 1.4.
Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya biashara nchini China, Yicai imesema kuwa dozi ya sindano nne za Wegovy itagharimu yuan 1,400 sawa na dola za Kimarekani 153 ($194).
Hatahivyo taarifa hiyo inasema kuwa watumiaji wa dawa hiyo watalazimika kulipia bei kamili ya dawa hiyo, kwani haijajumuishwa katika bima ya afya.
Utafiti unaonyesha kuwa watu wanene wanaotumia Wegovy wanaweza kupunguza uzito kwa zaidi ya asilimia 10% ya uzito wa mwili wao.
Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa China wa WeChat imesema dawa hii inauwezo mkubwa wa kutoa matibabu salama na bora ya kupunguza uzito kwa walio na uzito mkubwa.
Dawa ya Wegovy husaidia kudhibiti sukari, kupunguza hamu ya kula, na kuwafanya watu kujisikia kushiba.
Baadhi ya watafiti nchini humo wamedai kuwa dawa hiyo inaweza kuleta kichefuchefu na kutapika na pia watumiaji baada ya kuacha kutumia dawa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa wakurejea katika uzito wa awali.
Wegovy ilianza kuuzwa nchini Marekani mwaka 2021 na kuzua gumzo kubwa mitandaoni lakini dawa hii kwa sasa inapatikana katika maduka yote duniani
0 Comments