Dar es  Salaam .Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne na kidatu cha pili ,Takuwimu zikionyesha kwa darasa la nne wasichana wamefaulu zaidi ikilinganishwa na wavulana na kidatu cha pili wavulana ndio wameogoza.

Matokeo hayo yametangazwa leo Januari 4,2025 na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,Dk Said Mohamed mbele ya waandishi wa habari Akitangaza matokeo ya darasa la nne ,Amesema wanafunzi 1,320,227 kati ya 1,530,805 wenye matokeo sawa na asilimia 86.24,wamefaulu kuendelea na darasa la tano mwaka 2025 kwa  kupata madaraja A,B,C na D.

Aidha Akiendelea kusema matokeo hayo ni tafauti na mwaka 2023 ambapo wanafunzi waliofaulu walikuwa 1,287,934 sawa na asilimia 83.3.4,hivyo kuwa na ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.9 kwa wanafunzi waliopata fursa ya kuendelea na darasa la tano ikilinganishwa na mwaka 2023

Akiendelea kusema; Dk Mohamed amesema kati ya wanafunzi waliofaulu kuendelea na darasa la tano ,wasichana ni 699,901 sawa na asilimia 87.75 na wavulana ni 620,326 sawa na asilimia 84.61

Kwa upande wa kidatu cha  pili amesema ;wanafunzi 680,574 kati ya 796,825 wenye matokeo ambayo ni sawa na asilimia 85.41 wamefaulu kuendelea na kidatu cha tatu ambao wamepata madaraja ya 1,2,3 na 4 huku wavulana wakiongoza 

Amesema hii ni tafauti na mwaka 2023 ambapo wanafunzi waliofaulu wakiwa  592,741 sawa na asilimia 85 na kufanya ufaulu kuongezeka kwa asilimia 0.1

kwa matokeo hayo amesema ; kati ya wanafunzi 680,574 waliofaulu na kuendelea na kidatu cha tatu,wasichana ni 367,457 na wavulana  ni 313,117.