HABARI

6/recent/ticker-posts

DR.SAMIA AHIDI MAKUBWA ZAIDI KWA JAMII.


#HABARI YA KITAIFA

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Samia Suluhu Hassan Kupitia chama cha CCM, ameeleza kuwa vituo vya afya, hospitali za wilaya na rufaa tayari zimejengwa na kuwekewa vifaa vinavyohitajika na hivyo kuboresha huduma za afya nchini.
Akihutubia wananchi wa Mlowo Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya leo Septemba 4, 2025, Dkt. Samia amebainisha kuwa Serikali itawaajiri zaidi ya watumishi 5,000 wa afya katika kipindi cha siku 100 za mwanzo, ili kuongeza nguvu kazi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha, ameongeza kuwa wagonjwa wasio na uwezo, hasa wale wanaokabiliwa na magonjwa makubwa kama ya figo na moyo, wataendelea kupatiwa huduma stahiki na Serikali ili kuhakikisha wanapata huduma bila vikwazo.


Nikiripoti ni mimi Abrahmani Moh'd wa Tunaweza FM.






Post a Comment

0 Comments