Taasisi ya Tunaweza Arts Group yatangaza rasmin kuachilia nyimbo yao mpya ya Chama cha Mapinduzi itwayo " CCM CHAMA CHETU "Iliyoimbwa na wasanii wa Taasisi hiyo
Akizungumza Madam Aisha haji said ; Amesema Lengo la kuachilia nyimbo hiyo ni kuonesha wazi jitihada Alizozifanya raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Husein Ali Mwinyi ndani ya madaraka yake ya uraisi
Aidha Madam Aisha Haji Said akiendelea kusema ,Taasisi ya Tunaweza Arts Group inampongeza sana Dr . Husein Ali Mwinyi kwa kuifanya Zanzibar kuwa ya kipekee kwa kukuza uchumi wa nchi,watu kupata ajira na pia kuendeleza amani ya nchi
Taasisi hii , hufanya sanaa mbali mbali kama vile sanaa za maonesho ya jukwaani , Uimbaji wa nyimbo tafauti tafauti kwa lengo la kuelimisha jamii kutokana na mabaya yanayofanyika katika jamii yetu
Taasisi ya Tunaweza Arts Group inasema kuwa, Dr.Husein Ali Mwinyi ni Raisi mzuri na anasifa za kuongoza miaka mitano tena kwakutokana na umakini wa kazi anazozifanya na utu kwa wazanzibari.

0 Comments