HABARI

6/recent/ticker-posts

TAASISI YA TUNAWEZA ARTS GROUP YAFANYA ZIARA LEO.

UNGUJA

 Taasisi ya Tunaweza Arts Group leo yatembelea kikundi cha Sanaa ya uigizaji kiliopo Fuoni Birikani Unguja, kwa lengo la kuhamasisha Wasanii kutokata tamaa na kuamini sanaa ni kazi kama kazi nyengine.

Akizungumza katibu wa Taasisi ya Tunaweza, ndugu Abrahmani moh'd suleiman Akisema; Inapaswa wasanii kujuwa ndoto zao katika Uigizaji ili kuweza kufanikiwa kwa haraka katika Sanaa zao.

Aidha, nae Muhasibu wa Taasisi ya Tunaweza, Ughti Aisha Haji Said Akisema; Sanaa inahitaji moyo mkubwa ili ufanikiwe na kueka mbali mapenzi , kuheshimu viongozi wanaokuongoza na kuhuzuria mazoezi kila siku basi utaweza kuwa msanii mzuri na kufika mbali.





Post a Comment

0 Comments