Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, akiongoza kikao kazi cha kupitia sera ya mageuzi ya kimkakati katika sekta ya Utalii zanzibar
Yasemwa hayo leo Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege : upitishwaji wa sera mpya itasaidia kuondoa changamoto zilizokuwepo hapo awali kwa kuanzisha vyuo vya kutoa elimu kuhusiana na Utalii ili kuongeza Pato la Taifa
Aidha Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Abuod Suleiman Jumbe amefahamisha kuwa imefanya KAZI kubwa ya kuichambua sera iliyopo awali na kuangalia mapungufu na changammoto zilizomo ili kurekebisha changamoto hizo na sekta ya utalii izidi kukuwa kama raisi wa zanzibar anavyotaka.
Aidha amefahamisha kuwa sera hiyo itaweza kusaidia kukuza zaidi kwa soko letu la utalii na serikali kupata mapato ya asilimia 80.5 na pamoja kupata kipato kwa mtu binafsi
Aidha amefahamisha kutokana na mageuzi hayo ya kimkakati imepelekea kuifungua Pemba kiutalii na kujitokeza kwa wawekezaji mbalimbali kuunga mkono juhudi hiyo kwa kuzingatia maadili ya kizanzibari
.
Nao Washiriki wa kikao hicho wamesema kuwa sera hiyo itapewa kipaombele kwa wananchi kwani bila Elimu utalii utaporomoka na kupata kesi zisizozamsingi na jamii kukosa maendeleo .
0 Comments