Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu – Zanzibar alipozungumza na wajumbe kutoka Kamisheni ya Umoja wa Ulaya ukiongozwa na Bi. Rita Laraujinha Mkurugenzi Mwendeshaji wa masuala ya nje, Kanda ya Afrika.
Rais Dk. Husein Ali Mwinyi ameeleza kwa muda mrefu Zanzibar imekua ikipokea megawatt 100 za umeme kutoka Tanzania Bara kupitia waya za chini ya bahari ambao kwa sasa hautoshelezi, hivyo kuna kila sababu ya kupata umeme mbadala na kufikiria kuwa na umeme wa jua, mawimbi au upepo, hivyo ameuomba Umoja wa Ulaya (EU)kuangalia uwezekano wa kuisadia Zanzibar kwenye eneo hilo.
Aidha, alisema, Serikali inafikiria kuzisarifu taka kwaajili ya kupata umeme mbadala hatua aliyoielezea mbali yakupata nishati hiyo lakini pia itazizibiti taka kwani kumekua na changamoto kubwa ya usimamizi wa taka zinazozalishwa kila siku.
Pia vile vile Dk. Husein Ali Mwinyi ameeleza nia ya Serikali kuwaongezea nguvu, uwezo na utaalamu kwa wakulima wa mwani ambao asilimia 90 ni wanawake, kwa kuliinua zao hilo pamoja na kuanzisha viwanda vidogovidogo na vya kati ili kuusarifu na kuzalisha bidhaa zinazotokana na zao hilo
Aidha Akiendelea kusema; ameusisitiza Umoja wa Ulaya kuiungamkono Zanzibar katika azma yake ya kukuza Uchumi kupitia sekta za kimkakati ikiwemo Uchumi wa Buluu na Utalii ambazo ni Sekta za kipaumbele kwa Serikali anayoiongoza.
0 Comments