Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Chanjaani Jombwe Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za kutimia miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Aidha Akiendelea kusema: kazi kubwa imeshafanywa na Serilikal ya Awamu ya Nane (8) ya kuimarisha miundombinu ya elimu katika kila Wilaya Unguja na Pemba hivyo amewataka wananchi wa Jimbo la Kiwani kuwasimamia na kuwahimiza vijana katika suala zima la kuwapatia elimu ili kuweza kutoa wataalamu wengi na weledi watakaolisaidia na kuliongoza Taifa.
Pia vile vile : Amewataka wananchi wa Chanjaani Jombwe na maeneo jirani kuthamini maendeleo yanayoletwa na Serikali na Chama cha Mapinduzi kwa kuitunza miundombinu inayoendelea kujiunga ndani ya Jimbo lao ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kuwanufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.
Makamu wa Pili wa Rais amesema Serikali ipo katika mchakato wa kuzijenga barabara Kuu na Barabara za ndani kwa kiwango cha lami katika Wilaya ya Mkoani jambo litakalorahisisha upatikanaji wa huduma ya usafiri kukuwa kwa uchumi na kuongezeka kwa thamani kwa maeneo yote .
0 Comments