RAIS Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ni moja kati ya nchi 12 zitakazozindua mpango mahususi wa kitaifa kuhusu nishati za umeme Kupitia mpango huo unatarajia kuongeza kasi ya kuunganisha umeme nchini hadi kufikia asilimia 72 ifikapo mwaka 2030.
Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi Afrika unaoendelea muda huu ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam
Aidha RAISI Samia Suluhu Hassan Akiendelea kusema; kufanikisha azma hiyo ndani ya muda wa miaka mitano ijayo, tutahitaji uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 13, ambapo dola bilioni 5 zitapatikana kutoka sekta binafsi hapa nchini
0 Comments