Wananchi wa Mikoa mbali mbali ya Bara na Visiwani Zanzibar wamefanya maandamano yaliyoanzia Darajani Mjini Unguja hadi Forodhani kwa lengo la kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dkt Samia kwa kuuleta Mkutano wa Viongozi na Wakuu wa Nchi kwenye Mkutano wa Nishati

Mkutano huo mkubwa wa Wakuu wa Nchi uliofanyika kwa Siku mbili Tanzania uliojikita kujadili na kuweka maadhimio umekua wa kwanza huku ukiletwa na Rais  Mwanamke Tanzania

Wananchi wa Zanzibar wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mjini ,Asma Mwinyi ,Wadau na Wananchi wamefanya matembezi hayo huku wakibeba mabango  yenye picha za Viongozi na wakuu wa Nchi na Kisha kujiachia Forodhani wakiashiaria kuunga mkono jitihada za Rais.