BASI la New Force lililokuwa likitokea Tunduma kuelekea Dar es Salaam limepata ajali katika eneo la Bwawani, Chalinze mkoani Pwani baada ya kuacha njia na kugonga mti leo Februari 20, 2025 saa 11 asubuhi.
Akithibitisha kuwepo kwa ajali hiyo Kaimu Kamanda, ACP Muhudhwari Msuya amesema majeruhi waliopatikana ni 12 ambao waliofikishwa katika Hospitali ya Msoga kwa matibabu na majeruhi 11 tayari wameruhusiwa na alieyebaki hospitali ni mmoja ambaye anaendelea kupatiwa matibabu na hakuna hata mmoja kufariki
Inasemekana kuwa basi hilo likiwa barabarani ghafla liliacha njia na kwenda kugonga mti pembezoni mwa baarabara. Kwa upande wa majeshi hao wengine waliokuwa wamepona katika ajali hiyo walifikishwa na kuendelea na safari ya kuelekea kambini kwa kuenda kuendele na majukumu ya kujenga taifa.
0 Comments