#HABARI MKOA WA SINGIDA.
Mgombea Uraisi Dkt. Samia Suluhu Hassan Kupitia chama cha CCM, amesema ataendeleza kukuza Mazao mbali mbali na kuleta tija katika mkoa wa Singida .
Ameyasema hayo leo katika mkutano wake wa kampeni huko mkoa wa singida mjini Dkt Samia Suluhu Hassan amesema ataweza kutoa ruzuku ya mbolea ,na ataanzisha vituo mbali mbali za zana za kilimo ili wakulima wafanye kilimo chao bila ya Usumbufu wowote.
Aidha, Dkt.Samia akiendelea kusema ndani ya mkoa huwo ataweka kituo cha kupoozea umeme , miundombinu ya barabara yenye masafa ya kilomita 30.4 ambayo itafanyika katikati ya mkoa wa singida ili wakazi wa mkoa huwo wasafirishe mazao yao kwa urahisi kutoka shamban kuelekea sokoni.
NIKIRIPOTI NI MIMI ABRAHMANI MOH'D WA TUNAWEZA FM
.

0 Comments