HABARI YA KIGOMA
Jeshi la polisi la mkoa wa Kigoma wana utaratibu wa kutoa elimu ya masuala ya ulinzi na usalama hadi vijiweni kwa wananchi.
Amesema hayo kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Kigoma, Filemon Makungu amesema wananchi wa Kigoma sio wakaidi, wanatii
sheria bila shuruti pindi wanapoelimishwa masuala ya ulinzi na usalama, hali
ambayo amesema imeleta matokeo chanya kwa wananchi kutoa taarifa za uhalifu au
viashiria vya uvunjifu wa amani na wao hushughulika na suala hilo.
Aidha, kamanda huyo akisema akitoa mfano wa tukio la ujambazi lililotokea Kibondo mkoani humo ambapo wananchi walitoa taarifa na Jeshi la Polisi wakadhibiti tukio hilo na halikuleta madhara kwa wananchi.
NIKIRIPOTI NI MIMI ABRAHMANI MOH'D WA TUNAWEZA FM.

0 Comments