Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan amesema kipaumbele kikuu katika Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 kitakuwa utumiaji wa gesi asilia, ambapo jitihada zitalenga ukamilishaji wa mradi wa gesi asilia iliyoyeyushwa (LNG) wa Dola bilioni 42, ambao utaiweka nchi katika soko la nishati duniani
Akizungumza leo Dk Samia amefafanua taarifa hii alipozungumza na makamishna wakuu, mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa Ikulu ya Chamwino, Dodoma Wakati Dira 2050 ikielenga ukuaji wa uchumi wa tarakimu mbili kupitia ongezeko la tija katika kilimo na kuongeza thamani katika viwanda vyetu
Akiendelea kusema DK Samia; Serikali itazingatia ufunguzi wa fursa mpya za kiuchumi kupitia uchumi wa bluu, uchumi wa kijani, usafirishaji, na mazingira ya kidijitali ili kuweza kusaidia wananchi wetu wa Tanzania
Kwa upande mwingine, nchi inaendeleza mazingira yanayovutia uwekezaji, ubunifu, na kuongeza thamani ya ndani katika sekta muhimu ya madini Hatua zetu zitalenga kuendeleza uwekezaji unaohakikisha teknolojia za kesho, kusaidia mpito wa nishati safi duniani, kukuza viwanda, na kutoa faida za moja kwa moja kwa Watanzania
Pia vile vile; nao G20 wamefurahishwa na kuunga mkono kwa ajenda ya madini muhimu Tanzania inakubali kikamilifu mpango huu na ipo tayari kushirikiana na wadau wa kimataifa kuhakikisha rasilimali hizi zinachangia teknolojia safi duniani na ukuaji jumuishi hapa Tanzania.

0 Comments